This site uses cookies and similar technologies to store information on your computer or device. By continuing to use this site, you agree to the placement of these cookies and similar technologies.
Read our updated Privacy & Cookies Notice to learn more.
Out-of-date browser detected
Your browser appears to be out-of-date, and portions of the site may not function as intended.
Please install a current version of Chrome, Firefox, Edge, or Safari for a better experience.
Je Wanawake wanaweza kuwa nguzo kuu nchini Kenya, baada ya janga?

Nakala hii inapatikana pia kwa Kiingereza.
Licha ya sehemu ya ulimwengu unakozaliwa, maisha ni magumu zaidi iwapo unazaliwa ukiwa msichana. Hilo limekuwa ukweli daima, lakini hasa baada ya COVID-19.
Janga lilipoangusha uchumi, data ilionyesha kuwa wanawake walielekea kupoteza uwezo wao wa kuchuma mapato haraka zaidi ya wanaume. Na katika maeneo mengine ambako virusi viligharikisha mifumo ya afya, afya ya uzazi ya kinamama—sehemu ya mfumo iliyowatunza kinamama wajawazito—ilikuwa miongoni mwa za kwanza kutoweka.
Ulimwengu unahitaji mashirika zaidi yaliyojitolea kwa dhati kwa usawa wa kijinisa, hasa baada ya 2020. Hayo ndiyo maoni ya Bill & Melinda Gates Foundation, ambayo iliundwa miongo miwili iliyopita kwa wito wa kumpa kila mtu maisha yenye afya na hadhi. Baada ya miaka ya kazi ya kusikiliza na kujifunza kutoka kwa wataalamu, washirika, na jamii, ilikuwa wazi kuwa jinsia ilihitajika kuwa kipaumbele ili kuleta mabadiliko na fursa kwa nusu ya idadi ya watu duniani.
Wito huu umeelekeza Gates Foundation hadi Kenya, ambapo baadhi ya vikundi vyenye dhamira ya haki za raia vimejitolea kuwapa wanawake zaidi huduma wanazohitaji—na fursa wanazostahili. Vingi vinalenga afya, kama Jhpiego Kenya, iliyosaidia kuunda tume maalum ya kushughulikia mimba za ujana nchini na pia kusanidi nambari ya simu ya moja kwa moja katika Kaunti ya Kakamega; hivi, wanawake wajawazito wangeweza kupigia mtu simu kila wakati ili kupelekwa katika kituo cha afya.

Kwa miaka 20 iliyopita, Gates Foundation imekuwa na fursa ya kukutana na kusikiliza viongozi wa vikundi kama MamaYe na Jhpiego Kenya wanao tetea matumizi ya fedha za uma kwa afya wa wanawake. Na kwa sababu ya mazungumzo haya, sasa wakfu una uwezo bora zaidi wa kufadhili miradi inayowafaa wakenya—miradi kama Kangaroo Mother Care, njia ya kuwafundisha kinamama wageni. Watoto wachanga, hasa wale wadogo sana, wanahitaji kuwekwa joto; la sivyo huenda wanaweza kufa. Wafanyakazi wa afya ya kijamiii wamewaonyesha maelfu ya kinamama wa Kenya mbinu rahisi ambayo haihusishi chochote zaidi ya kutumia kitambaa ili kumfuga mtoto wao ili awe karibu na mwili wao kupata joto. Wameona jinsi kugusana kwa ngozi huboresha afya ya watoto na maisha ya kinamama, sababu iliyofanya Gates Foundation kusaidia kufadhili juhudi yao.
Kazi hii inaleta mafanikio nchini Kenya. Kuanzia 2010 hadi 2019, vifo vya kinamama wanapojifungua vilipungua kwa zaidi ya asilimia 9 na vifo vya watoto waliozaliwa karibuni vilipungua kwa asilimia 17.

Juhudi za kuboresha maisha ya wanawake ni pana kuliko afya. Nchini Kenya, kuna miradi ya kuwasaidia wakulima wa kike na wengine ili kutoa akaunti za kuweka akiba za kidijitali zilizoundwa mahsusi kwa ajili ya wanawake ili waweze kudhibiti fedha zao. Jinsi miradi hii inavyozidi kupanuka na kufanikiwa, jamii nzima huelekea kuona thamani yake; sio wanawake pekee huona hili bali wanaume pia.
Kwa hakika, utafiti unaonyesha kuwa wanawake wanapokuwa na fursa zaidi—na uwezo wa kudhibiti pesa zao, hasa—wana uwezekano mkubwa wa kuwekeza katika maeneo wanakoishi na hasa kwa watoto wao. Mwanamke aliye na pesa mikononi mwake na uwezo wa kuamua matumizi yake, ni mwanamke ambaye anaweza kuchagua atakacho fanya na maisha yake na kutekeleza shughhuli na fursa za kutosheleza. Wanawake wanapowezeshwa kiuchumi, thamani huboreka. Wanakuwa na nguvu zaidi na sauti.
Hii ndiyo sababu inayoifanya Gates Foundation kufadhili kazi za usawa wa kijinsia: Huanzisha kipindi cha mambo adilifu yanayojirudia. Watoto wanapolishwa vyema na kuweza kwenda shuleni, hufanikiwa. Watoto wanapofanikiwa, familia na jamii hunufaika.
Ulimwengu una matatizo mengi sana kwa nusu ya nguvu na uwezo wa kiakili wa dunia kufungiwa kwenye nafasi zisizo muhimu. Wanawake wanaweza kuisaidia Kenya—na ulimwengu—kujijenga upya baada ya janga hili. Wao sio waathiriwa tu wa ulimwengu usio na usawa; wanawake pia wanaweza kuwa nguzo kuu nchini Kenya.
Masasisho katika tovuti yetu
Asante kwa kutembelea ukurasa huu. Sehemu kubwa ya tovuti yetu ipo kwa Kiingereza pekee kwa sasa. Tunaendelea na mchakato wa kusasisha maudhui yetu ili kutoa lugha nyingine.
Kuhusu Gates Foundation
Kwa kuongozwa na imani kuwa kila maisha yana thamani sawa, Bill & Melinda Gates Foundation hufanya kazi ili kuwasaidia watu wote kuishi maisha yenye afya na fanifu. Katika nchi zinazostawi, ingalenga kuboresha afya ya watu na kuwapa fursa ya kujiondoa kwenye njaa na umaskini uliokithiri. Ndani ya Marekani, inanuia kuhakikisha kuwa watu wote—hasa wale walio na rasilimali chache zaidi—wanafikia nafasi wanazohitaji ili kufanikiwa shuleni na katika maisha. Ukiwa na makao ndani ya Seattle, Washington, na ofisi kote duniani, wakfu huu unaongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu Mark Suzman, chini ya uelekezi wa Bill na Melinda Gates na Warren Buffett.
Published 1/26/21